348. Kweli Yahuisha
1. Kweli yahuisha,
Maneno yenye uzima,
Muda unatosha,
wewe uweze kukoma.
Ni faida gani,
Wapata kwake Shetani?
Geukeni kwa Yesu rudini,
atakuponya dhambini.
Ee ndugu
muda wako unapita.
Ya kale yageuka na kupita.
Yale mapya
ndiyo sasa tunapata.
2. Wafikiri nini, wewe usipofuata
mafunzo ya dini,
kama ulivyoyapata?
Mchana u mwema,
usiku unageuka. Shika maonyo
vema daima, utaona ni baraka.
Ee ndugu …
3. Ni huzuni sana,
kwa watu wengi wa Mungu,
kwa kutokazana
kuyafuata ya mbingu.
Wasikia mengi,
nao wayaacha tena.
Lakini kwa dhambi zao nyingi
wanatengwa naye Bwana.
Ee ndugu …
4. Ajabu ni wazi,
wengi waona aibu,
Kuifanya kazi ya Bwana
mwenye thawabu.
Wajificha wengi,
watenda kimataifa.
Wenzangu, ndiyo huzuni nyingi
ya kuelekea kufa.
Ee ndugu ...
5. Maisha ya wengi,
sasa wakata tamaa.
Uzito ni mwingi,
moyoni wajitetea.
Waona machozi,
hao wote wenye dhambi.
Kumbuka imemalizwa kazi.
Yesu ameshinda dhambi.
Ee ndugu ...
6. Yesu alifika
kwa watu kuwakomboa.
Naye husikika pengi
katika dunia.
Na kila namna ya watu
anawatunza. Atoaye
wokovu ni Bwana
kwa kuwa huwaongoza.
Ee ndugu …