354. Mteteeni Yesu
1. Mteteeni Yesu, mlio askari;
Inueni beramu, mkae tayari;
Kwenda naye vitani,
sisi hatuchoki
hata washindwe pia
Yeye amiliki.
2. Mteteeni Yesu, vita ni vikali;
Leo siku ya Bwana,
atashinda kweli;
Waume twende naye,
adui ni wengi
lakini kwake Bwana
tuna nguvu nyingi.
3. Mteteeni Yesu, wenye ushujaa;
Nguvu zenu za mwili
hazitawafaa;
Silaha ya Injili vaeni daima;
Kesheni mkiomba;
msirudi nyuma.
4. Mteteeni Yesu, vita ni vikali,
wengi wamdharau,
hawamkubali,
ila atamiliki
tusitie shaka,
kuwa naye vitani
twashinda hakika.