356. Njia Ile Nyembamba
1. Njia ile ni nyembamba
ya uzimani.
Heri anayefuata njia ile tu.
Ee nishike
(Bwanangu nishike Bwana)
nifike kwa Bwana.
(uzimani tu kwa Bwana)
Wewe ndiwe njia.
2. Heri anayeamini asipoona.
Atapata kufahamu
yasiyoonwa.
Ee, nishike …
3. Angalia ni mzima
aliyekufa,
Hivyo sote tu wazima
tukimwamini.
Ee, nishike …
4. Ee, mwenzangu ukiomba
unikumbuke,
Niwe hai tangu sasa
na Yesu Kristo.
Ee, nishike …