373. Nyumbani, Nyumbani
1. K: /: Nyumbani,
W: Nyumbani
ni Yerusalemu:/
K: Ndipo mahali,
W: Ndipo mahali niendapo.
K: Jamani,
W: Jamani ninakwenda,
/: Natamani makao ya
Yerusalemu. :/
2. K: /: Kesheni,
W: Kesheni siku itakuja. :/
K: Tutaonana,
W: Tutaonana na Bwana
K: Vizuri,
W: Vizuri kumtazama,
/: Tumtazame Mwokozi
mwenye utukufu. :/
3. K: /: Kwa Yesu,
W: Kwa Yesu nimetumaini. :/
K: Twende zetu, wee,
W: Twende zetu,
wee mwenzangu.
K: Upesi,
W: Upesi kwake yeye.
/: Namchungulia Yesu,
kule kwenda kukaa. :/
4. K: /: Njia hii,
W: Njia hii tunayofuata :/
K: Ya kutazama,
W: Ya kutazama popote.
K: Mwenzangu,
W: Mwenzangu, usiache. /:
Utazame njia hii
itupelekayo. :/
5. K: /: Ni wengi
W: Ni wengi
waliotakaswa.:/
K: Wanamsifu,
W: Wanamsifu na jeshi.
K: Duniani,
W: Duniani wamepona.
/: Ndiyo wenye vilemba
wenye kuingia. :/
6. K: Wang’aa,
W: Wang’aa
washindao tamaa, :/
K: Kama umeme
W: Kama umeme wang’aa
K: Ni kweli,
W: Ni kweli washindao,
/: Kama nguo za nyota,
kama za umeme. :/
7. K: /: Na huko,
W: Na huko
ndiko hamu yangu. :/
K: Asili yangu,
W: Asili yangu kwa
Mungu
K: Tazama,
W: Tazama enzi yake.
/: Maumivu na hofu
yameachwa huko. :/
8. K: /: Edeni,
W: Edeni ni kwenye uzima:/
K: Atawalaye,
W: Atawalaye ni Mungu.
K: Bwanangu,
W: Bwanangu, nijalie.
/: Nivutie mbinguni
kunako uzima.:/