403. Katika Neema ya Yesu
1. Katika neema ya Yesu
nimeokolewa,
nilipotea dhambini,
kipofu rohoni.
2. Bali neema ya Yesu
yanitosha sana
ilinifumbua macho
ikanifungua.
3. Nilikuwa mwenye hofu
nilifungwa nazo,
nimefunguliwa sasa
kwa neema ya Yesu.
4. Nitamsifu Bwana wangu
maishani mwote,
kwani nina ushirika
Msalabani mwake.
5. Tutakapofika wote
mbinguni kwa Mungu,
tutashukuru neema
ya Yesu milele.