399. Hata Ndimi Elfu
1. Hata ndimi elfu elfu,
/:Hazitoshi kweli:/
Bwana Yesu kumsifu,
Kwa zake fadhili. X3
2. Yesu jina liwezalo
/:Kufukuza hofu:/
Lanifurahisha hilo,
Lanipa wokovu. X3
3. Jina hilo ni uzima;
/:Ni afya; amani:/
Laleta habari njema;
Twalipiwa deni. X3
4. Yesu huvunja mapingu
/:Ya dhambi moyoni:/
Msamaha, tena nguvu,
Twapata Rohoni. X3
5. Kwa sauti yake vile
/:Wafu hufufuka:/
Wakafurahi milele,
Pasipo mashaka. X3
6. Ewe Yesu wangu Bwana
/:Uwezo nipewe,:/
Kuhubiri kote sana,
Wote wakujue. X3