384. Mungu Akitupa Kipaji

1.  Mungu akitupa kipaji 

    kilicho kizuri zaidi

    atusafirisha duniani,

    tuone mazuri yake.


2.  Mwoga hataki kwenda mbali,

    hupenda kuwa kwao tu,

    afanana na vifaranga 

    wasiotoka kwa mama.


3.  Mito yaporomoka sana

    na ndege wanaimba juu,

    tunashirikiana nao

    kwa furaha za mioyo.


4.  Mungu wetu na asifiwe!

    Hulisha ndege, wanyama,

    dunia na mbingu ni zake,

    yee hatatusahau nasi. 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya