424. Nionapo Amani Kama Shwari

1. Nionapo amani kama shwari,

   Ama nionapo shida; 

   Kwa mambo yote umenijulisha

   Ni salama rohoni mwangu 

         Salama rohoni, 

         Ni salama rohoni mwangu

   

2. Ingawa Shetani atanitesa, 

   Nitajipa moyo kwani 

   Kristo ameona unyonge wangu,

   Amekufa kwa roho yangu  

           Salama rohoni …


3. Dhambi zangu zote,

   wala si nusu, 

   Zimewekwa Msalabani; 

   Wala sichukui laana yake,

   Ni salama rohoni mwangu  

            Salama rohoni …


4. Ee Bwana, himiza siku ya kuja;

   Panda litakapolia;

   Utakaposhuka sitaogopa;

   Ni salama rohoni mwangu. 

            Salama rohoni… 


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya