427. Sioni Haya kwa Bwana

1.  Sioni haya kwa Bwana

    Kwake nitang’ara! 

    Mti wake  sitakana 

    Ni Neno imara  

         Msalaba ndiyo asili 

         ya mema  

         Nitatua mzigo hapo; 

         Nina uzima, furaha daima, 

         Njoni kafurahini papo


2.  Kama kiti chake vivyo, 

    Ni yake ahadi,

    Alivyowekewa navyo,

    Kamwe havirudi

          Msalaba ndiyo asili …


3.  Bwana wangu, tena Mungu,

    Ndilo lake jina! 

    Hataacha roho yangu, 

    Wala kunikana 

          Msalaba ndiyo asili …


4.  Atakiri langu jina 

    Mbele za Babaye

    Anipe pahali tena 

    Mbinguni nikae 

           Msalaba ndiyo asili...


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya