436. Yesu Aliniita, "Njoo"

1. Yesu aliniita, “Njoo,

   raha iko kwangu;

   Kichwa chako ukilaze 

   Kifuani mwangu”

   Nilikwenda kwake mara, 

   sana nilichoka;

   Nikapata kwake raha,

   na furaha tena.


2. Yesu aliniita, “Njoo, 

   kwangu kuna maji; 

   Maji ya uzima, bure,

   unywe uwe hai”

   Nilikwenda kwake mara 

   na maji nikanywa: 

   naishi kwake, 

   na kiu kamwe sina tena.


3. Yesu aliniita,” Njoo, 

   dunia ni giza, 

   Ukinitazama nuru takung’arizia”

   Nilikwenda kwake mara

   Yeye jua langu, 

   ni kila wakati mwanga

   safarini mwangu.