419. Ni Nguvu Ituongozayo

1.  Ni nguvu ituongozayo 

    wote sasa (milele) 

    Ni nguvu itokayo juu

    Kwa Baba Mungu, ya uzima.

    Mimi sina kitu kistahilicho 

    Ee Mwokozi (ila mimi) mimi,

    nitumike, Katika kazi yako

    ya uzima ningalipo hai.


2.  Utupe vipawa toka kwako 

    mbinguni (daima)

    Ni nguvu itokayo juu

    tushukiayo daima. 

    Tubariki sisi sote 

    Mwokozi maishani 

    Mimi (hata mimi)

    nitumike katika kazi 

    yako ya uzima ningalipo hai


3. Tuvike utakatifu 

   wako Bwana ee (twaomba)

   Tuvike uwezo wako 

   ulio hai, tuhuike.

   tubariki sisi sote

   Mwokozi maishani. 

   Sisi (hata sisi) tutumike, 

   katika kazi yako

   ya uzima tungalipo hai.


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya