425. Shusheni Nyavu Zenu

1. “Shusheni nyavu zenu 

    Palipo maji mengi 

    Mtapata mavuno,”

    Bwana amesema: 

    Simoni akasita,

   “Mbona tumesumbuka 

   usiku kucha bure” 

   :/: Akasema, Nenda!:/:


2. Ee Bwana umesema, 

   tukawavue watu 

   vilindini mwa dhambi

   za ulimwengu huu. 

   Simoni akasita,

   “Mbona tumesumbuka 

    Usiku kucha bure; 

   :/:Nami nitakwenda!”:/:


3. Simoni alipata 

   baraka za ajabu 

   aliposhusha nyavu

   katika bahari. 

   Ee Bwana twakuomba

   Utujalie nasi, 

   Tufanye upendavyo:

   :/:siku zetu zote:/:


4. Sisi sote Wakristo

   tushushe nyavu zetu,

   tukawavue watu

   waje kwa Mwokozi.

   Kwa jina lake Yesu

   hatutazipoteza 

   Baraka toka Mungu:

   :/:Sifa zake Bwana!:/:


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya