426. Sifuni Mungu
Sifuni Mungu
kwa maana yeye
ni mwenye pendo kuu.
Sifuni Mungu kwa
maana yeye ni mkuu
1. Ameturuzuku yeye pekee
kwa yanayofaa; kwetu ni nafuu.
Ameturuzuku yeye pekee
kwa yanayofaa:
ni ya neema tu.
Sifuni Mungu...
2. Kamtuma Mwokozi bila mawaa,
kutoa balaa na hata fadhaa.
Kamtuma Mwokozi bila mawaa,
kutoa balaa ni ya neema tu.
Sifuni Mungu...
3. Na tumtumikie kwa kila saa,
bila kukataa wala kunyamaa.
Na tumtumikie kwa kila saa,
bila kukataa ni ya neema tu.
Sifuni Mungu...