428. Tangu Siku Hiyo
1. Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu,
Sina giza tena ila mwanga pia
Kwa Yesu Mwokozi wangu.
Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu;
Sina shaka kamwe
kwa sababu Yeye
Yu nami moyoni mwangu.
2. Sina haja tena ya kutangatanga,
Ndiye kiongozi wangu,
Dhambi zangu zote
zimeondolewa,
Na Yesu, mwanawe Mungu.
Amani moyoni …
3. Matumaini yangu ni ya hakika,
katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu
zimeondoka
kwa kuwa ninaye Yesu
Amani moyoni …
4. Siogopi tena nikiitwa kufa,
Yu nami daima, Yesu.
Mlango wa mbinguni
ni Yeye pia,
“Tapita humo kwa damu”
Amani moyoni …
5. Nitaketi na Yeye huko milele,
Nisifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote
Kwa Yesu, Mwanawe Mungu
Amani moyoni…