430. Tufani Inapovuma
1. Tufani inapovuma
Sana moyoni mwangu,
Huona pa kujificha
Mkononi mwa Mungu
Hunificha, hunificha
Adui hatanipata,
Hunificha, hunificha,
Mkononi mwake.
2. Pengine kuna taabu
Yanisongeza kwake;
Naijua si hasira,
Ni ya mapenzi yake.
Hunificha, hunificha...
3. Adui wakiniudhi
Nami nikisumbuka,
Mungu atavigeuza
Vyote viwe baraka.
Hunificha, hunificha...
4. Niishipo duniani
Ni tufani daima,
Anilindapo rohoni
Nitakaa salama.
Hunificha, hunificha...