431. Tukutane Kila Upande
1. Tukutane kila upande
Tusikie ya mbinguni
Tunataka kusikia
ya uzima wetu;
Twatazama Goligota
alipotufia
:/:Twende (Twendeni)
Pale (Goligota)
Alipoinuliwa:/:
2. Macho yetu yaelekezwa
kutazama ya rohoni.
Unavuta watu kwako
toka kila ‘pande;
Kutazama Goligota ulikotufia
:/: Twende (twendeni)…
3. Ewe roho unyenyekee,
ya mbinguni yakujie
Jipunguze, jipunguze ili ye azidi:
Mtafute, mtafute
Rafiki wa mbingu.
:/: Twende (twendeni)…