432. Atukuzwe
(Atukuzwe), atukuzwe
Mwokozi wetu,
(Atukuzwe), atukuzwe
mwokozi wetu,
1. Wote waliofungwa
awafungua,
Wote wenye njaa
awapa chakula.
(Atukuzwe)...
2. Wote waliao
awapa faraja,
Wote waumwao
anawatuliza
(Atukuzwe)...
3. Wote wateswao
nguvu atawapa,
Wote wapigwao
atawashindia.
(Atukuzwe)...
4. Wote wamwitao
ataitikia,
Wote waaminifu
taji atawapa.