433. Tumeingia Sisi Katika Nyumba Yako
1. Tumeingia sisi
katika nyumba yako.
Tumekuja kuomba,
kwako ee Mungu wetu.
(Hakika) takatifu
(Nyumba hii) yako Bwana
(Ee Mungu) wa upendo
Mungu mwenye upendo.
Tukaribishe Bwana,
nasi utubariki.
Kama unavyofanya,
kwa watu wako wote
2. Mwangaza wako Bwana
umetakasa nyumba.
Kwa nuru yako Bwana,
nyumba ni takatifu
(Hakika) takatifu …
3. Mungu Baba na Mwana
na Roho Mtakatifu.
Pokea nyimbo zetu,
na maombi pokea.
(Hakika) takatifu …