434. Umechoka, Umeshushwa Moyo?
1. Umechoka, umeshushwa moyo?
Mwambie Yesu, mwambie Yesu;
Una huzuni, huna furaha?
Mwambie Yesu sasa.
Mwambie Yesu,
mwambie Yesu,
Amejulika sana;
Hayuko rafiki kama Yesu,
Mwambie Yesu sasa.
2. Unalia juu ya haja zako?
Mwambie Yesu, mwambie Yesu;
Mbona wazificha dhambi zako?
Mwambie Yesu sasa.
Mwambie Yesu ...
3. Waogopa? Usihuzunike,
Mwambie Yesu, mwambie Yesu;
Una hofu kwa mambo ya mbele?
Mwambie Yesu sasa.
Mwambie Yesu...
4. Waogopa uwazapo kifo?
Mwambie Yesu, mwambie Yesu;
Wautamani ufalme wake?
Mwambie Yesu sasa.
Mwambie Yesu...