438. Yesu Zamani Bethelehemu

1. Yesu zamani Bethilehemu

   Aliyezaliwa kwa aibu, 

   Ndiye Mwokozi wa ulimwengu,

   Akaja kwa mimi.

      Akaja kwa mimi;

      Akaja kwa mimi;

      Ndiye Mwokozi wa ulimwengu,

      Akaja kwa mimi.


2. Yesu akafa Msalabani, 

   Kuniponya akalipa deni, 

   Ni la ajabu la jinsi gani 

   Kunifia mimi!

       Kunifia mimi! Kunifia mimi!

       Ni la ajabu ya jinsi gani

       kunifia mimi!


3. Ni Yeye huyo tangu asili:

   Na nilipotangatanga mbali

   alikuja kwa upole, kweli 

   Kuniita mimi!  

        Kuniita mimi! 

        Alikuja kwa upole, 

        kweli kuniita mimi!


4. Yesu Kristo atarudi tena,

   hilo lanifurahisha sana,

   Yeye Bwana akionekana 

   Kunijia mimi.

         Kunijia mimi, kunijia mimi. 

         Yeye Bwana akionekana 

         Kunijia mimi. 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya