440. Zaeni Matunda Mema
1. Zaeni matunda mema;
Zaeni matunda yale,
Zaeni yenye Baraka;
Zaeni ya heri.
Bwana akiyapokea
Yatabarikiwa sana.
Zaeni matunda mema,
Zaeni ya Heri.
2. Safisha matendo yako
Safishwa mwenendo
wako.
Safishwa na Bwana Yesu.
Safishweni nyote.
Bwana akiyapokea…
3. Fanyeni kazi kwa moyo
Fanyeni kwa kupatana
Fanyeni na Bwana Yesu.
Fanyeni kiroho.
Bwana akiyapokea…